Highlands FM

Kudungwa na nyuki kivutio kipya cha utalii tiba asilia Mbeya

4 September 2025, 12:37

Afisa Nyuki TFS, Agnetha Luoga. Picha na Samwel Mpogole

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS limeendelea kuwa kivutio baada ya kuongezwa zao jipya la utalii.

Na Samwel Mpogole

Katika hali isiyozoeleka lakini yenye mvuto wa kipekee, wananchi na wageni wamefurahishwa na huduma ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS inayotolewa katika Shamba la Miti Kawetire lililopo mkoani Mbeya kwa ajili ya kuhudumiwa na nyuki, wakidungwa maksudi kwa lengo la kupata faida za kiafya, huku hatua hiyo ikitajwa kuwa sehemu ya vivutio vipya katika kukuza utalii wa tiba asilia nchini.

Afisa Nyuki katika shamba hilo, Agnetha Luoga, anasema zoezi hilo la kudungwa na nyuki limekuwa likifanyika kwa hiari ya mtu binafsi, ambapo anaelekezwa kisha kuruhusiwa kudungwa katika maeneo maalum ya mwili ili kusaidia mzunguko wa damu, kuondoa maumivu ya viungo, pamoja na kuamsha kinga ya mwili.

Sauti ya Agnetha Luoga

Kwa upande mwingine, hatua hiyo imevutia pia sekta ya utalii Hozza Mbura, Afisa Utalii Mwandamizi ambaye pia ni Mkuu wa Kanda wa Bodi ya Utalii – Nyanda za Juu Kusini, amesema matumizi ya nyuki kama sehemu ya tiba na kivutio cha utalii ni ubunifu unaopaswa kuungwa mkono, kwani unaongeza wigo wa utalii wa kipekee nchini.

Sauti ya Hozza Mbura

Wananchi waliodungwa na nyuki nao wametoa maoni mbalimbali, wengi wakieleza walivyojionea nafuu katika miili yao.

Sauti ya wananchi

Kwa hali hiyo, zoezi la kudungwa na nyuki katika Shamba la Miti Kawetire linatajwa si tu kuwa mbinu ya tiba asilia, bali pia fursa ya kipekee katika kukuza utalii wa tiba nchini, huku likibaki kuwa kielelezo cha ubunifu wa matumizi ya rasilimali za misitu kwa manufaa mapana ya jamii.