Highlands FM
Highlands FM
1 September 2025, 12:25

Jamii imetakiwa kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali nchini ili kujifunza na kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Na Samwel Mpogole
Jamii imekumbushwa kuendelea kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii ili kujifunza, kuburudika na kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza na kituo hiki, Veronica Jacob Paul, Msimamizi wa Hifadhi ya Ifisi Zoo iliyopo Mbalizi, anasema hifadhi hiyo ina nafasi kubwa katika kutoa elimu na kuongeza mwamko wa jamii kuhusu thamani ya wanyama na vivutio vya asili.
“Hifadhi hii inawakaribisha wananchi na wadau wote. Tunataka jamii itambue kuwa utalii siyo burudani pekee, bali ni elimu na njia ya kuendeleza uhifadhi kwa vizazi vijavyo.”
Nao baadhi ya wadau waliotembelea hifadhi hiyo wamesema uwepo wa maeneo kama haya ni fursa nzuri ya kutanua maarifa na kujipumzisha.
“Tumejifunza mambo mengi, hasa kuhusu wanyama. Ni sehemu nzuri ya kutembelea na familia kwa ajili ya elimu na mapumziko.”
Ifisi Zoo inabaki kuwa moja ya vivutio vinavyoongeza hadhi ya Mkoa wa Mbeya katika kukuza utalii wa ndani na kutoa fursa kwa jamii kuenzi urithi wa mazingira.
