Highlands FM

Wakulima waaswa kuzingatia ulinzi wa mazingira

6 August 2025, 13:01

Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bakari Mwaruma.Picha Samwel Mpogole

Wakulima mkoani Mbeya wametakiwa kuzingatia ulinzi wa mazingira ili kusaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Na Samwel Mpogole ..

Wakulima mkoani Mbeya na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini wametakiwa kuzingatia ulinzi wa mazingira licha ya shughuli zao za kilimo, ili kusaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bakari Mwaruma, amesema baadhi ya shughuli za kilimo zimekuwa chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira.

Sauti Bakari Mwaruma,
Afisa Mazingira Mwandamizi wa NEMC, Mbeya. Tilisa Mwambungu

Kwa upande wake, Afisa Mazingira Mwandamizi wa NEMC, Mbeya. Tilisa Mwambungu, amesema wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira.

Sauti Tilisa Mwambungu

NEMC imewataka viongozi wa vijiji na kata kushirikiana kikamilifu katika kutoa taarifa za uharibifu wa mazingira ili hatua stahiki zichukuliwe mapema.