Highlands FM
Highlands FM
24 July 2025, 12:34

Wasimamizi wa Uchaguzi Mkoani Mbeya Wametakiwa kusimamia viapo vyao na kuwa wasiri kwenye kipindi hiki cha uchaguzi ili kuepuka migogoro.
Na Samwel Mpogole
Wasimamizi wa uchaguzi wametakiwa kuwa waaminifu, kutunza siri za kazi, na kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ikiwemo magroup ya WhatsApp ili kulinda uadilifu wa mchakato wa uchaguzi.
Wito huo umetolewa na Afisa Mwandamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi, Daniel Kalinga, aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Jakub Mwambeghele, wakati wa kufunga semina ya mafunzo ya uchaguzi kwa watendaji kutoka mikoa ya Mbeya na Songwe.
Kwa upande wake, Afisa Mwandamizi kutoka Tume huru ya uchaguzi, Phiner Kidunda, aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Tume hiyo, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyojifunza ili kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa weledi na uaminifu.
Sauti Phiner Kidunda
Naye Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, Bw. Gideon Mapunda, amesema mafunzo yamekuwa na tija kubwa na kwamba watendaji waliopata mafunzo hayo wako tayari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa katika kipindi cha uchaguzi.
