Highlands FM

Wafanyabiashara Mbeya waomba kasi iongezeke ujenzi wa barabara.

2 July 2025, 13:26

Katibu tawala mbeya Rodrick Mpogolo.Picha Samwel Mpogole

Wafanyabiashara na wadau mbalimbali mkoani mbeya wameiyomba serikali mkoani mbeya kuharakisha ujenzi wa barabara ili waendeleze shughuli zao.

Na Samwel Mpogole

Wito huo umetolewa katika mkutano uliohusisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma, ambapo Rose Muliahela kutoka Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) amesema ucheleweshwaji wa kukamilika kwa mradi wa barabara ya njia nne umeendelea kuathiri shughuli za kibiashara, hususan katika maeneo ya pembezoni mwa mji.

Sauti Rose Muliahela

Akijibu hoja hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Ndugu Rodrick Mpogolo, amesema Serikali imeshaanza kuchukua hatua mbalimbali za kushughulikia changamoto hizo, ikiwemo ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi na kuendeleza kazi za ujenzi katika maeneo tofauti ya mkoa.

Sauti Rodrick Mpogolo