Highlands FM
Highlands FM
1 July 2025, 13:11

Wananchi wametakiwa kutoa taarifa za wanyamapori wakali ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza
Na Samwel Mpogole
Jamii, hususani wakazi wa maeneo yanayopakana na hifadhi za taifa, wametakiwa kuhakikisha wanatunza mazingira na kutoa taarifa mapema mara tu wanapoona au kuhisi uwepo wa wanyamapori katika makazi yao ili kuepusha madhara kwa binadamu na wanyama hao.
Wito huo umetolewa na Bw. Lameck Kidava, mwongoza watalii kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, wakati akizungumza na Highlands FM radio ameelezea umuhimu wa ushirikiano baina ya wananchi na mamlaka za uhifadhi huku akisisitiza kutunzwa kwa mazingira kwaujuma.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliotembelea hifadhi hiyo wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuongeza juhudi za pamoja katika kulinda na kuhifadhi mazingira ya hifadhi. Wamesisitiza kuwa uhifadhi bora ni kichocheo kikubwa kwa maendeleo ya sekta ya utalii na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii nchini Tanzania, na ni rasilimali muhimu inayohitaji ulinzi wa pamoja kati ya serikali, wananchi na wadau wa mazingira.
