Highlands FM

Dawa za kulevya zinavyoua ndoto za vijana Mbeya

18 June 2025, 18:06

Afisa DCEA, Adrick Ndelwa. Picha na Samwel Mpogole

Vita dhidi ya dawa za kulevya, Ni sauti za waliopitia giza la uraibu, zikiifumbua  macho jamii kuhusu mateso, upweke, na matumaini mapya

Na Samwel Mpogole

Baadhi ya waraibu wa dawa za kulevya jijini Mbeya wameiomba serikali kuongeza nguvu katika kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo haramu, wakieleza kuwa matumizi yake yameendelea kuwa chanzo cha mateso, unyanyapaa na kupoteza mwelekeo wa maisha kwa vijana wengi nchini.

Wakizungumza na Highlands FM,  waraibu hao ambao kwa sasa wanaishi katika nyumba ya upataji nafuu ya Southern Highlands Sober House mkoani Mbeya, wameelezea madhila waliyopitia kutokana na matumizi ya dawa hizo, ikiwemo kupata matatizo ya afya ya akili. Wametumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa vijana wenzao kujiepusha na vishawishi vya kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.

Sauti za waraibu

Salum Nasolo Salum, ambaye ni kijana aliyewahi kuwa mraibu na kwa sasa ndiye mmiliki wa nyumba ya upataji nafuu ya Southern Highlands Sober House, ameeleza kuwa sababu nyingi zinazopelekea vijana kuingia kwenye matumizi ya dawa hizo zinatokana na malezi duni, huku akisisitiza umuhimu wa familia kujenga misingi bora kwa watoto wao.

Sauti ya Salum Nasolo Salum

Kwa upande wake, Onesmo Mwihava, Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Empower Care Foundation, inayojihusisha na utoaji wa elimu na huduma za kisaikolojia kwa waraibu na makundi rika, ameeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika juhudi za kusaidia waraibu kuacha matumizi ya dawa hizo.

Sauti ya Onesmo Mwihava

Nao Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kupitia kwa Afisa wake Adrick Ndelwa na Queen Komba, imesema kuwa juhudi za mamlaka hiyo zimeendelea kuzaa matunda kwa kushirikiana na vyombo vya usalama, jamii na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupambana na biashara na matumizi ya dawa hizo.

Sauti ya Adrick Ndelwa na Queen Komba

Pamoja na changamoto zilizopo, wadau mbalimbali wameendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ambapo uwepo wa DCEA katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini umeongeza ufanisi wa mapambano hayo.

Queen Komba Afisa DCEA, Picha na Samwel Mpogole