Highlands FM
Highlands FM
13 June 2025, 12:31

Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kimetoa utaratibu wa kuchukua fomu kwa ngazi za ubunge na udiwani.
Na Mwanaisha Makumbuli
Katibu wa siasa na uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa Mbeya Christopher Uhagile ametoa utaratibu wa kuelekea mchakato wa uchaguzi wa Madiwani na Wabunge.
Uhagile amesema hayo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za ccm zilizopo sokomatola jijini mbeya ambapo ametaja mwelekeo na nafasi za wajumbe wanne ambao wameonesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali.
Aidha uhagile amesema kuwa mchakato wa utoaji fomu kwa nafasi za udiwani na ubunge utaanza Juni 28,2025 na kuwataka wanachama kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu za chama hicho.
