Highlands FM

NEMC Yaonya Kelele na Matumizi Haramu ya Plastiki

27 May 2025, 19:10

Meneja NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Josiah Murunya. Picha na Samwel Mpogole

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa onyo kali kwa wote wanaokiuka taratibu za utunzaji wa mazingira, hususan kwa kuzalisha kelele kupita kiasi na kutumia mifuko ya plastiki isiyo sahihi

Na Samwel Mpogole

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka wafanyabiashara na wananchi wote wanaojihusisha na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama “Lambo”, kuacha mara moja, huku likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka agizo hilo.

Wito huo umetolewa na Meneja wa NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Josiah Murunya, alipokuwa akizungumza na Hope Channel ofisini kwake jijini Mbeya. Amesema matumizi ya plastiki hiyo yameendelea kuathiri mazingira kwa kiwango kikubwa na kwamba Baraza hilo halitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Sauti ya Josiah Murunya akielezea tatizo la mifuko ya plastiki

Katika hatua nyingine, Murunya ameonya jamii kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kudhibiti viwango vya kelele, hasa katika maeneo ya makazi, biashara na burudani, kwa kufuata kikamilifu kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali.

Sauti ya Josiah Murunya akielezea tatizo la kelele

Baraza hilo limeendelea kutoa elimu na kusisitiza ushirikiano wa jamii katika kuilinda ardhi, maji na hewa dhidi ya uchafuzi unaoweza kuepukika kwa hatua madhubuti.