Highlands FM
Highlands FM
23 May 2025, 17:43

Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo jipya la Uyole mkoani Mbeya katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu
Na Thobias Mgimwa
Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo jipya la Uyole mkoani Mbeya katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini, leo Ijumaa Mei 23, 2025, Dk Tulia ametumia nafasi hiyo kuwapa nasaha kwa wananchi hao na kwa mgombea ajaye katika uchaguzi huo.
Licha ya kutangaza kugombea katika jimbo la uyole Dr Tulia ameahidi kuendelea kuwasaidia wananchi wa jimbo la mbeya mjini katika Nyanja mbalimbali.
Hii imekuja baada ya Tume huru ya uchaguzi kuridhia ombi la kugawanywa kwa jimbo la Mbeya na kupatikana jimbo jipya la Uyole Mapema mwezi Mei.
