Wakulima wa pareto mkoa mbeya na songwe watakiwa kuzingatia ubora wa uzalishaji wa zao hilo.
31 May 2024, 17:19
Pareto ni moja kati ya zao la kibiashara ambalo hulimwa mikoa sita tu nchini tanzania, zao hilo ni jamii ya maua hutumika kutengenezea dawa za kuuwa wadudu.
Na Lameck Charles
Highlands Fm Radio
Serikali ya Wilaya ya Mbeya imesema itaendelea kuhakikisha zao la pareto linakuwa bora kwa kuhakikisha wanunuzi wanafuata utaratibu uliopo ili kuepuka na hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya vishoka wa zao hilo.
Rai hiyo imetolea na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa wakati akizungumza na wanunuzi wa makampuni ya pareto wa mikoa ya Mbeya na Songwe.
Aidha Beno Malisa amesema wilaya ya Mbeya ina kampuni tisa za ununuzi wa zao hilo la kibiashara na kuzitaka kampuni hizo kuwajibika kwa kulipa kodi za halmashauri kwa lengo la kuleta maendeleo ya halmshauri husika.
Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa makapuni ya ununuzi wa pareto ikiwemo kampuni ya PCT wamesema msimu uliomalizika walipata hasara kutokana na ununzi wa maua yasiyokidhi viwango hivyo ni matumaini yao misimu ujao wa mavuno watanunua maua yaliyo bora ikiwa ni kuwaelimisha wakulima na mawakala wao.
Lucas Ayo ni Mkurugenzi wa wa Zao la pareto Tanzania amewasihi wanunuzi wa zao la pareto kushikamana na kuwa pamoja kwa utekelezaji waliyokubaliana ikiwemo kuto nunua maua yasiyo kauka.
Kikao hicho kilichokaliwa kwa lengo la kufanya tathmini ya zao la Pareto huku hali ya uzalishaji wa zao hilo ikipanda kutoka tani elfu mbili hadi kufikia tani elfu nne kwa sasa.