Highlands FM

Kuelekea siku ya mazingira duniani jamii imeaswa kuendelea kutunza mazingira

30 May 2024, 17:27

Afisa Mazingira Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira  NEMC  Kanda ya Nyanda za juu kusini TILISA MWAMBUNGU

Na Lameck Charles

Highlands Fm Radio

Kuelekea siku ya Mazingira Duniani jamii imeaswa kuendelea kutunza Mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi  yanayoweza kutokea kutokana na Uharibifu wa Mazingira.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Mazingira Baraza la Taifa  la Uhifadhi na Usimamizi na Mazingira  NEMC  Kanda ya Nyanda za juu kusini TILISA MWAMBUNGU wakati akizungumza na kituo hiki Kwenye  maonesho ya Mbeya Expo 2024  ambapo amesema kila mwananchi ana wajibu wa kutunza mazingira yanayomzunguka.

Sauti Tilisa Mwambungu

Aidha amesema kuelekea June 5 siku ya Mazingira Duniani Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini  litazindua wiki ya Mazingira ambapo mgeni rasmi anataraji kuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dr Tulia Ackson.

Sauti Tiliza 2