Wananchi Mbeya watoa maoni kuhusu faida, fursa ya zao la nyuki
20 May 2024, 17:09
Ufugaji wa nyuki unaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato cha ziada kwa wakulima wadogowadogo. Uzalishaji wa asali nchini Tanzania umekuwa ukitegemea sana wafugaji wadogowadogo, wanaotumia njia za kiasili kama vile mizinga ya magogo au vyungu, kwa nyuki wa kiafrika ambao ni wengi sana kwenye mapori.
Na John Ilomo
Ikiwa leo ni siku ya nyuki duniani wananchi mkoani Mbeya wametoa maoni yao kuhusu faida na fursa ya zao la nyuki katika maisha ya kila siku.
Wakiongea na kituo hiki wananchi hao wamesema kuwa hawana mazoea ya kutumia zao la nyuki ambayo ni asali kutokana na ukosefu wa elimu kutoka kwa wataalam wa bobezi wa masuala ya nyuki.
Kwa upande wake mfanyabiashara anyejishughulisha na uuzaji wa bidhaaa zinazotokana na nyuki Judika Kibona amesema kuwa zao la nyuki ni muhimu kwa binadamu kwani hutumika kama tiba lakini pia nyuki mwenyenye ni chanzo cha mapato kwa wafanyabishara wa zao hilo.
Bi. Kibona ameelezea namna alivyosukumwa kujihusisha na sekta hiyo kufuatia mwitikio wa watumiaji wa asali mkoani hapa.
Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 20 mwezi Mei kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kitaifa imefanyika Dodoma ikiwa na kaulimbiu isemaye “Nyuki kwa Afya na maendeo Tuwatunze”.