Highlands FM

Kamati CST yaja na mipango mikakati kukabiliana na vitendo vya ukatili

17 May 2024, 18:21

Mkuu wa Idara ya Miradi ya Child Support Tanzania {CST} Hildergade Mehrab .

Watoto wanapitia changamoto nyingi miongoni mwa walezi wao na wanajamii. Kutokana na yale wanayoyapitia pamoja na mazingira duni wanamoishi, watoto wengi hukosa mwelekeo thabiti wa kimaadili hivyo basi kukosa mahitaji yao ya kuwawezesha kuwa na hulka zinazokubalika katika jamii kila mmoja.

Na Lameck Charles

Kamati ya Miradi ya CST imekaa kikao na kuangazia miradi iliyotekelezwa kwa mwaka mmoja uliopita ikiwa ni pamoja na masuala ya ulinzi na usalama kwa watoto na kujadili wajibu wa kila mwanakamati katika miradi mipya inayotarajiwa kufanyika.

Akizungumza katika kikao hicho Hildergade Mehrab ambaye ni mkuu wa idara hiyo amesema kuwa kutokana na kushamiri kwa matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto kila mwanakamati ana jukumu la kuhakikisha suala la ulinzi na usalama kwa watoto linapaziwa sauti kwa lengo la kutokomeza matukio hayo ya kikatili.  

Sauti ya Hildergade Mehrab

Hildergade amewataka wananchi na wahanga wanaofanyiwa vitendo vya kikatili kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za kikatili pasipo kuhofia kutambulika kwani taarifa hizo zitapokelewa na kushughulikiwa kwa usiri mkubwa huku akiwaomba wadau wanaopokea taarifa hizo kuendelea kutengeneza mifumo salama kwa ajili ya mwananchi anayetoa taarifa hizo.

Sauti ya Hildergade Mehrab

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Damasi Saimon Mwambeje amebainisha miradi waliyonayo kwa sasa ambayo ni “pelekea rafiki zangu shuleni”  pamoja na mradi wa kutembelea mikoa ya Rukwa, Songwe na Katavi ambapo amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya miradi hiyo kwa lengo la kuwafikia watoto wengi ili kuwawezesha kupata afua stahiki zao muhimu za kielimu.

Sauti ya Damasi Saimon Mwambeje

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho akiwemo Mwashele Ayubu ambaye amemwakilisha mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kyela iliyopo wilaya ya Kyela amesema kuwa shule yake ni moja ya shule iliyonufaika na ukarabati wa miundombinu ya watoto wenye ulemavu na hapa anaeleza.

Sauti ya mwalimu Mwashele Ayubu

Kamati ya miradi ya Child Support Tanzania ni kamati inayofanya vikao vyake kila baada ya miezi 6.