Tumbatu FM
Tumbatu FM
10 November 2026, 09:54

Picha ya Mkurugenzi wa jumuiya ya vijana na elimu kaskazini A” Unguja JUVIEKA Ndugu Mbarouk Maalum Mohamed, picha na Atka Mosi Makame
“Kuna haja ya kuweka uwiano wa majukumu kwa watoto nyumbani kama vile kuchota maji,kufua,kupika,kuosha vyombo,na kuchanja kuni ili kuwasowesha kuwa na uwajibikaji wa pamoja.”
Na Atka Mosi Makame
Mkurugezi wa jumuiya ya vijana na elimu Mkoa wa kaskazini Unguja JUVIEKA Mbrouk Maalum Mohamed amesema ipo haja ya wazazi kuzingatia usawa wa haki za jinsia katika kugawanya majukumu ya kazi kwa watoto wao majumbani ili kuondosha mitazamo dhaifu kwa jamii ya kwamba watoto wakiume hawapangiwi majukumu ypypyte.
Hayo ameyasema mara baada ya kumaliza mafuzo yaliyofanyika katika ukumbi wa skuli ya secondary Mkokotoni yaliandaliwa na JUVIEKA kwa kushirikiana na FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY ambapo amesema lengo la mafuzo hayo ni kutengeneza mikakati ya kuleta usawa wa kijinsia kwa kugawanya majukumu kwa mtoto wa kiume na wakike ikiwemo kuchota maji,kufua,kupika,kuosha vyombo,na kuchanja kuni nk.
Maalum ameeleza kua majukumu yanapokua mengi kwa mtoto wa kike akiwa na umri mdogo hunapelekea athari tofauti ,ikiwa ni pamoja kukosa muda mzuri wa kujisomea ,kupumzika,na hata kukosa muda wa kukaa pamoja na wazazi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Aidha amesema wazazi wanapaswa kusaini majukumu ya kazi na watoto wao ili kuwaweka imara na kuwasimamia kupigania haki za kuishi na kugawanya majukumu yatakayo saidia kuondosha ukandamizaji na mifumo dume kwa mtoto wa kike.
Sauti ya Mkurugenzi wa jumuiya ya vijana na elimu kaskazini A” Unguja JUVIEKA Ndugu Mbarouk Maalum Mohamed
Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya kaskazi A” Makame Haji amesema mafuzo hayo yanaendana na uhalisia katika jamii , hivo wataendelea kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha wanaifikisha elimu hiyo kwa jamii ili kusaidia kuleta uwiyano wa fursa na upatikanaji wa haki kwa jamii.
Nae Msaidizi wa sheria Wilaya ya kaskazini A Unguja Salama Ibrahim Juma amesema wazazi wanatakiwa kuwafahamisha watoto wa kiume kazi za lazima ambazo watu wote wanafanya bila kubebeshwa jinsia fulani au mtu mmoja mmojaKwa upande waKE mwalimu wa skuli ya Mapindui secondary Bakari Ali makame na mwalimu wa madrasakutoka Mkokotoni Bi Amina kadiri wameishukuru jumuiya hiyo kwa kuwapatia mafuzo na kuahidi kuyafanyia kazi katika sehemu zao za kazi na na kwa jamii ,huku wakiwataka wazazi kuacha ubaguzi wa malezi kwa mtoto bali wawape wakati sahihi wa kutafuta elimu itakayo saidia kuleta kheiri kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mafuzo hayo ya siku mbili yaliyoshirikisha washiriki 20 kutoka taasisi za serikali, asasi za kiraia walimu pamoja na viongozi wa dini.