Tumbatu FM

Viongozi Tumbatu watakiwa kuwajibika

21 September 2026, 12:56

Picha ya pamoja kati ya Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi ( watatu kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wakati wakikuagua Hospitali ya Wilaya Tumbatu kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo jimbo la Tumbatu. (Picha na Vuai Juma)

“Jamii inaweza kunufaika na uwepo wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika maeneo yao ikiwa wasimamizi watawajibika ipasavyo” (Ni kauli ya Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi)

Na Vuai Juma

Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar wametakiwa kusimamia majukumu yao ili kurahisisha upatikanaji wa hudumu ndani ya jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanizibar Abdi Mahamoud Abdi huko katika Hospitali ya Wilaya ya Tumbatu wakati wa ziara maalum ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kujenga uhai wa chama hicho.

Amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa lengo la kuondoa usumbufu wa huduma za kijamii hivyp utendaji mbovu wa viongozi unapelekea kutofikiwa malengo hayo huku akiwataka kujitathimini sambamba na kubadilika kivitendo.

Ni sauti ya Naibu Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi akihimiza uwajibikajikwa viongozi

Kwaupande mwengine  katibu tawala Wilaya ndogo Tumbatu Khatib Habib Ali amesema  lengo la kujengwa Hospitali hiyo ni kuondoa changamoto ndogo ndogo za kiafya na inategemewa kuwahudumia wakazi wa shehia Nne za Kisiwa cha Tumbatu baada ya kukamilika kwake.

Ni katibu tawala Wilaya ndogo Tumbatu Khatib Habib Ali anaefafanuwa lengo la kujengwa Hospitali ya Wilaya ndogo Tumbatu

Nae Daktari dhamana Wilaya ya Kaskazini  “A” Himidi Juma Saidi  ameeleza kuwa kabla ya kujengwa kwa kituo hicho watu wa Tumbatu wamelazimika Kwenda kivunge kwaajili ya matibau hivyo kumaliza kwa ujenzi huo kutachangia kuondosha usumbufu mkubwa kwani wanategemea kutoa huduma za kibingwa huku akiwahimiza wakazi wa maeneo Jirani na kisiwa cha Tumbatu kuitumia fursa hiyo.

Sauti ya Daktari dhamana Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja Dokta Himidi Juma Saidi akizungumzia juu ya watu wa Tumbatu walivyokuwa wakisumbuka kutafuta huduma za Afya nnje ya Tumbatu