Tumbatu FM

TCRA Zanzibar yahimiza matumizi ya leseni kidijitali

16 November 2023, 3:28 pm

Picha ya meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA Zanzibar) Picha na Makame Pandu.

“Matumizi sahihi ya hudma za kimtandao yataepusha makoza yanayojitokeza kwa watumiaji.”

Na Makme Saplaya.

Vijana wa mkoa Kaskazin Unguja wametakiwa kuwa wabunifu katika matumizi ya mitandao ya simu kwani kupitia mitandao hiyo kuna fursa nyingi zitakazowapatia tija na waache kukaa kwenye vijiwe kupiga soga zisizo na maana yeyote.

Hayo ameyasema Bi Esuvatie Masinga ambaye ni Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Zanzibar wakati akiwa kwenye kipindi maalum na Redio Jamii Tumbatu cha kutoa elimu kuhusu leseni kidijitali na klabu za kidijitali.

Amesema ujio wa leseni hizo pamoja na klabu kidijitali ni fursa pekee kwa vijana ya kujiingizia kipato ambacho kitawasaidia katika maisha yao.