Tumbatu FM

Wizara ya afya zanzibar yafanya muendelezo wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi

12 November 2023, 11:34 am

Picha ya Wazriri wa Afya Zanzibar akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Najing ya nchini China kuhusiana na zoezi la uchunguzi WA shingo ya kizazi. Picha na Habari maelezo

“Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya ugonjwa hatari sana hivyo ni vyema kutokomezwa”

Na Vuai Juma

Wizara ya Afya Zanzibar kupitia Kitengo cha Maradhi yasiombukiza  kwa kushirikina na Serikali ya China jimbo la Jiangsu wamefanya muendelezo wa kambi ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi  katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

Waziri wa Wizara hiyo  Nassor Ahmed Mazrui amesema katika kuimarisha Afya za Wananchi  zoezi hilo litaendelea kufanyika kwa lengo la kutatua changamoto hiyo kwa akinamama Nchini.

Alifahamisha kuwa zoezi hilo lina lengo la  kuangalia maambukizi ya shingo ya kizazi dhidi ya ugonjwa wa saratani na kutoa matibabu Kwa wale wote watakaobainika kuwa na ugonjwa huo ndani na nje ya Nchi  bila malipo . 

 Kwa upande wake  Meneja wa maradhi yasiombukiza Zanzibar Dkt Omar Mohamed Suleiman alisema zoezi kama hilo linatarajiwa kusogezwa Kwa jamii Kwa kuwafikia akina mama katika maeneo mbalimbali ikiwemo  vikosi vya SMZ na SMT pamoja na baadhi ya Vyuo vikuu hivyo aliwataka akina mama hao kuitumia vyema fursa hiyo pale itakapowafikia.

Zoezi hilo  linaloendeshwa na wataalamu wa hapa nchini kwa kushirikiana na madaktari kutoka China ni la  tano kufanyika Visiwani Zanzibar.