Tumbatu FM

Tumbatu kunufaika na mradi wa maji baada ya kukamilika

16 November 2023, 4:02 pm

Picha ya Tangi la maji lilojengwa tumbatu ambalo linauwezo wa kuingia lita milioni moja.

Picha na Vuai Juma

Kukamilika kwa mradi kutapunguza tatizo la maji kisiwani tumbatu kwa kiasi kikubwa.

Picha ya katibu tawala Tumbatu akiambatana na viongozi wengine katika ukaguzi wa miradi.(Aliyechuka mwevuli wa Zantel) Picha na Vuai Juma.

Changamoto ya huduma ya maji safi na salama kisiwani tumbatu inatarajiwa kupungua kwa kiasi kikubwa baada ya kukamilika mradi wa maji kisiwani humo.

Hayo yamesemwa na katibu tawala wilaya ndogo tumbatu Khatib Habib  Aly wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya kimaendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya ccm kupitia serekali ya mapindunduzi ya Zanzibar na yaJamauhuri ya muungano wa Tanzania ambayo inalengo la kuwaondoshea wakazi wa kisiwa cha tumbatu changamoto mbali mbali zinazo wakabili.

Amesema ujenzi wa mradi wa tangi la maji lenyeuwezo wa kuhifadhi lita milioni moja kwasasa ujenzi wake umeshakamilika na tayari tangi hilo limesha kabidhiwa malaka ya maji Zanzibar Zawa kwaajili ya kumalizia hatua zilizobakia za kuunganisha mabomba ndani ya visima kutoka Donge kipange hadi tumbatu kazi ambayo imekwishaanza.

Aidha amesema kwasasa hudma ya maji inapatikana ingawa ni kwakiasi kidogo kutokana na tangi hilo kuwa katika hatua za majaribiao huku akizaitaja shehia za Gomani na Mtakuja kuwa ni waathirika zaidi  wa ukosefu wa maji hali inayochangiwa na kuchakaa kwa miundombinu ya ya zamani inayosambaza hudma hiyo.

Sauti ya katibu tawala wilaya ndogo Tumbatu.

Picha ya Mradi wa jengo la shule ya sekondari inayotarajiwa kuwa na gorofa 3 litakapo kamilika.

Picha na Vuai Juma

Kwaupande wake Mkandarasi wa miradi inayotekelezwa Kisiwani Tumbatu kutoka kampuni ya Simba Devloper  John Simo amesema wanakabiliwa na changamoto za usafirishaji wa vifaa vya ujenzi kutokana na hali ya kimazingira ya kisiwa hicho samabamba na uwepo wa mvua kwa wakati huu jambo ambalo linawafanya kutotekeleza kazi zao kwa wakati.

Sauti ya mkandarasi kutoka kampuni ya Simba Devloper John Simon.

Picha ya mkuu wa idara ya Siasa na Uhusiano wakimataifa kutoka ccm Zanzibar (Aliyepo kati na Kati) picha na Vuai Juma

Nae Mkuu wa idara ya Siasa na uhusiano wa kimataifa kutoka ofisi ya ccm Zanzibar  Rukia Salum Ali amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo huku akitoa pongezi kwa raisi wa Zanzibar kwa kuamua kwa maksudi  kupeleka miradi hiyo kwa watu wa tumbatu ambayo itakuwa ndio chachu ya maendeleo.

Miradi iliyo kaguliwa ni pamoja na mradi wa tangi la maji ujenzi wa skuli ya sekondari ya gorofa tatu eneo la ujenzi wa jingo la hospitali yenyehadhi ya wilaya pamoja na kituo cha polisi.