Tumbatu FM

Jumuiya ya Nataraji yatakiwa kujiepusha na masuala ya kisiasa

3 December 2023, 1:14 pm

Picha ya wanachama wa jumuiya ya Nataraji ya kisiwani Tumbatu wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza na uzinduzi wa jumuiya yao. Na Vuai Juma.

Kuanzishwa kwa jumuiya ambazo zitaepukana na aina yoyote ya uchochezi kutachangia kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika jamii.

Na Vuai Juma.

Wanachama wa Jumuiya ya Nataraji  Social Development Foundation  wametakiwa kucha tabia ya ubaguzi  wa kisisa ndani  na nnje ya jumuiya yao ili kuweza kufikia malengo yao kwa haraka.

Wito huo umetolewa na muwakilishi wa jimbo la tumbatu ambaye pia ni mshauri wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika masuala ya kisiasa muheshimiwa Haji Omar Kheir wakati wa uzinduzi wa jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa skuli ya sekondari Tumbatu.

Amesema jumuiya nyingi  hazifikii malengo kutokana na wanachama wake kuingiza  masuala ya kisiasa ndani ya jumuiya zao  hivyo nivyema  wanajumuiya hiyo kutokubali  kuruhusu  masuala hayo kwani hayana faida yoyote.

Aidha amewataka viongozi  wanaosimamia  jumuiya hiyo kujiepusha na matumizi mabaya ya  fedha jambo ambalo linapekeea migogoro ya muda mrefu .

Sauti ya Mh.Haji Omar.

Picha ya Mh. Haji Omar wakati akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa jumuiya ya Nataraji Social Development foundation ya kisiwani Tumbatu.

Picha na Vuai Juma.

Kwaupandewake katibu tawala wilaya ndogo Tumbatu Khatib Habib Aly amesema jumuiya hiyo imeanzishwa wakati sahihi kutokana na mahitaji yaliyopo kwa watu wa tumbatu na kuahidi kuwa itatoa mashirikiano makubwa kwa harakati zote sambamba na kusisitiza  suala la kuwaungwanisha watu wote wa tumbatu ili waweze kuepukana na masuala ya uchochezi.

Sauti ya Katibu tawala wilaya ndogo Tumbatu.

Kuwepo wa viongozi ambao wanashirikiana na taasisi binafsi kunapelekea kurahisisha majukumu ya tasisi hizo.

Picha na Vuai Juma.