Tumbatu FM

Wanafunzi Tumbatu washauriwa kuchunguuza afya zao.

12 November 2023, 11:16 am

Picha ya wanafunzi wa skuli ya sekondari Tumbatu. Na Vuai Juma.

Na Vuai Juma

Wanafunzi Kisiwani Tumbatu wameshauriwa kuwa na tabia ya kuchunguuza afya zao mara kwa mara ili kuweza kufahamu mwenendo wao wa kiafya.

Ushauri huo umetolewa na Daktari  kutoka kituo cha afya Tumbatu Gomani Dokta Mcha Haji Mkame wakiti alikpokuwa akitoa elimu juu ya afya ya uzazi na maradhi ya ukwimwi kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Tumbatu.

Amesema kuwa vijana wengi wamekuwa hawana tabia ya kwenda kuchunguuza afya zao jambo ambalo limekuwa likichangia pakubwa uwepo wa idadi kubwa ya watu wasiojua afya zao mapema nakupelekea kuathiriwa na maradhi katika miili yao bila wenyewe kujijua.

Akijibu swali lililoulizwa na wanafunzi hao kuhusu njia za maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mototo Dokta Mcha Amesema maranyingi mototo huambukizwa wakati akiwa tumboni, mama anapojifungua pamoja na mototo anaponyonyeshwa.

Sauti ya Dokta Mcha Haji kutoka kituo cha afya Tumbatu Gomani

Kuwepo kwa muendelezo wa elimu ya afya hasa mashuleni kutapelekea kutengeneza jamii iliyo bora na kuwahamasisha vijana wengi kupima afya zao”

Nao wanafunzi waliopatiwa elimu hiyo wamesema wataifanyia kazi taaluma waliyo patiwa kama inavyo takiwa ili kutengeneza jamii ambayo inaafya iliyobora.