Tumbatu FM

Tadio yatoa mafunzo kwa radio za kijamii Zanzibar

10 August 2023, 8:47 am

Picha ya Hilali Ruhundwa mhariri wa TADIO (aliye simama mbele) kwenye mafunzo ya waandishi wa habari. Picha na Vuai Juma.

Kuchapisha tarifa katika mtandao wa radio TADIO kutaongeza idadi ya wafuatiliaji wa tarifa za radio za kijamii.

Na Vuai Juma.

Wandishi wa habari wa radio za kijamii Zanzibar wametakiwa  kuitumia fursa ya kutuma kazi zao katika mtandao wa radio tadio  ili ziweze kuwafikia watu wengi kote ulimwenguni.

Hayo yamesemwa na mhariri wa mtandao huo Hilali Ruhundwa  mara baada ya kufunga mafunzo ya siku mbili kwa  radio za kijamii zilizo chini  Tadio kwa kanda ya Zanzibar yaliyokuwa na lengo la kuwaelimisha namna ya  kuchapisha habari kwenye mitandao yaliyofanyika ukumbi wa mikutano ZSSF Kariakoo Zanzibar.

Amesema kwa sasa mambo ya uandishi wa habari yamekuwa yanabadilika kila wakati hivyo ni lazima wanahabari wawe wanapatiwa elimu ili waweze  kuendana na mabadiliko hayo.

Sauti ya Mhariri wa radio TADIO Halali Ruhundwa.

Naye Katibu Mtendaji wa TADIO ndugu Ali Khamis amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa vyombo vya habari hasa vya kijamii lakini bado baadhi yao vimekuwa vikishindwa kutuma kazi zao kwenye mtandao kutokana na kukosa gharama za bando  pamoja na utafutaji wa habari huku akivitaka vyombo hivyo kujitahidi kulingana na uwezo wao.

Sauti ya Katibu Mtendaji wa TADIO ndugu Ali Khamis