Tumbatu FM

Wazazi, walezi Tumbatu watakiwa kutoa ushirikiano kwa walimu

9 August 2023, 1:59 pm

Wanafunzi wakiwa katika hafla ya utowaji wa zawadi. Picha Na Latifa Ali

Uwepo wa mashirikiano kati ya wazazi na walezi kutaongeza idadi ya ufaulu.

Na Latifa Ali

Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika  skuli ya msingi “B” kisiwani tumbatu wameatakiwa  kushirikiana na walimu wa skuli hiyo  ili kuhakikisha  wanafunzi wanasoma  na kufaulu katika masomo yao.

Wito huo umetolewa na katibu tawala wa wilaya ndogo Tumbatu  Khatib Habib Aly katika hafla ya kuwazawadia wanafunzi walio faulu mitihani ya taifa ya darasa la saba  kwa mwaka 2022 kwa skuli za msingi  za Tumbatu Gomani.

Aliesema  suala la mashirikiano baina ya wazazi na walimu ndio njia pekee ya kuwafanya wanafunzi waweze kusoma vizuri  nakuifanya skuli hiyo  iwezekupasisha wanafunzi wengi Zaidi katika mitihani yao.

Aidha aliwataka wanafunzi hao kuacha tabia ya kuwadharau walimu  nakuwahimiza wazingatie wanachofundishwa ili waje kuwa viongozi wazuri wa baadae.

Nae kaimu mwalimu mkuu  wa skuli hiyo ndugu Adam Shame  amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana katika mwaka uliopita bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwarudisha nyuma ikiwemo ukosefu wa vifaa vya matumizi ya ofisi,maabara ,vyoo Pamoja na eneo la akiba kwaajili ya matumizi ya skuli hivyo ameiomba wizara ya elimu Zanzibar pamoja na wadau wa elimu kusaidia kuzitatua changamoto hizo ili wapige hatua katika malengo yao waliyo jiwekea.

Zaidi ya wanafunzi 20 wamezawadiwa zawadi mbali mbali katika hafla hiyo ambazo zimetolewa na uongozi wa jimbo la tumbatu kwa kushirikiana wa walimu wa skuli hiyo.