Tumbatu FM

Ongezeni jitihada kwenye masomo ili kupata ufaulu mzuri

8 May 2026, 11:17

Ni picha ya mstahiki meya wa Baraza la Manispaa kaskazini “A” Unguja Nyange Kheir Ali akiwa na wananchi katika mahafali ya Skuli ya Sekondari Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja ( Picha na Mwahawa Hassan)
“Wazazi ni wajibu wenu kuwasimamia watoto ili waelekeze nguvu zao kwenye masomo waepuke vishswishi vibaya kwamanufaa yao ya baadae

Na Mwanahawa Hassan.

Mstahiki meya wa Baraza la Manispaa kaskazini “A” Unguja Nyange Kheir ambae pia ni diwani wa wadi ya Gamba amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao.

Ameyasema hayo wakati wa sherehe ya mahafali ya kuwazawadia wanafunzi waliofaulu katika mitihani yao ya kidato cha pili cha tatu na cha nne katika skuli ya sekondari ya matemwe Mkoa wa kaskazini Unguja kwa mwaka 2025.

Amesema jamii nyingi zilizokua zinaishi ukanda wa pwani zilikuwa na tabia ya kubeza suala la elimu lakini kutokana na juhudi za walimu kushirikiana na wazazi zimeongeza muamko wa suala kwa na kushajihika kuwapeleka watoto wao Skuli ili kupata elimu bora.

Picha ya mwalimu mkuu wa Skuli ya Sekondari Matemwe Sheha Mgasho (alievaa Koja Shingoni) akiiwa anahutubia kwenye mahafali ya Skuli yake ya Matemwe) (Picha na Mwanahawa Hassan)

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Skuli ya sekondari ya Matemwe Makame Sheha Mgasho ametoa shukrana kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwawekea miundombvinu bora ya elimu kwa mtaala mpya wenye kozi ya utaliii sayansi jamii pamoja na lugha ya kifaransa ambay ambao utamsaidia mwanafunzi pindi akimaliza masomo kuweza kujiajiri mwenyew bila ya kutegemea ajira serekalini.

Aidha amesme katika harakati za kutafuta elimu ni lazima kuwepo na mashirikiano ya pamoja kati ya  walimu wazazi kamati za skuli viongozi wa shehia na jimbo jambo ambalo litawasidia wanafunzi kusoma kwa ufanisi huku akiomba kuengezewa walimu wa somo la Kiingreza Hisabati Jiografia Historia na komputa application ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu vizur kwenye masomo yao.

Akisoma risala mwanafunzi wa skuli hiyo Tatu Khamis Mossi amesema skuli yao imepata mafanikio makubwa lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile uchache wa walimu wa sayansi ukosefu wa maktaba ya kisasa mazingira duni ya kambi na vifaa vya komputa.