Tumbatu FM

ZRA yatoa sadaka ya ftari kwa kaya 130 za Tumbatu

3 March 2026, 17:43

Picha ya wananchi wa Tumbatu wakiwa na watendaji wa mamlaka ya mapato Zanzibar (ZRA) kwenye zoezi la utowaji wa msada wa chakula kwa wakazi wa shehia za Tumbatu. (Picha na Juma Haji)

“ZRA imekua na tabia ya kurejesha kwa jamii fungu linalotokana na kodi za wananchi ili kuona kwa kiasi gani wananufaika na kodi ambazo wanalipa kwa serikali”

Na Juma Haji.

Ujumbe wa Mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA umefika Kisiwani Tumbatu na kugawa vyakula vya ftari kwa wananchi 130 wenye hali duni katika kisiwa hicho.

Akikabidhi msaada huo kwa wananchi kamishina wa mmlaka ya mapato Zanzibar Shaaban Jaffar Jumanne amewataka wananchi kuongeza wingo wa kudai rist kila wanapofanya malipo ili kuwezesha malaka kukushanya mapato zaidi ambayo yanatumika kukuza maendeleo na kutoa misaada kama hiyo katika jamii.

Amesema jukumu la kudai rist ni jukumu la kila mwananchi hatua ambayo hutoa msaada mkubwa kwa mamlaka hiyo katika kufuatilia mianya ya upotevu wa kodi ikiwemo baadhi ya wananchi kufanya mauziano bila ya kudai au kutoa rist.

Amewataka wananchi kuongeza kasi ya kudai rist katika kipindi hiki cha mataarisho ya matumizi ya sikukuu ili kurahisisha makushanyo ya fedha kutoka kwa wananchi.

Ni sauti ya kamishina wa Mamlaka ya mapato Zanzibar Shaaban Jaffar Jumanne.

Akijumuika na wananchi wa Tumbatu katika kupokea sadaka hiyo katibu tawala Wilaya Ndogo Tumbatu Khatibu Habibu Ali ameoupongeza uongozi wa mamlaka ya mapato Zanzibar kwa kuwafikishia vyakula hivyo na kusema kuwa vitasaidi kupata ftari.

Sauti ya Katibu tawala na wananchi wa Tumbatu wakizungumza wakati wakipokea msada wa chakula kwaajali ya futari ya ramadhani.

Wakati huo huo mamlaka hiyo imeendesha kipindi maalum cha elimu ya mlipa kodi kupitia Radio Jamii Tumbatu ili kuhakikisha inatimiza wajibu wake wa kutoa elimu kwa wateja wake waliopo vijijini.

Wakizungumza na wananchi kupitia kipindi hicho maafisa kutoka mamlaka ya mapato Zanzibar Bi Rahma Yussuf Habibu na Bw Abdl-shakur Ramadhan Simai wamesema ZRA hutumia vyobmbo vya habari kama ni jukwaa la kufikisha taarifa zake kwa wananchi ili kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma zake ndani ya jamii kwa urahisi.

Wamesema katika faida inayopatikana kwenye makushanyo ya Mamlaka, wamekuwa wakiunga mkono miradi mbali mbali  ya kijamii na ile ya kitaifa ikiwemo miradi ya shule, barabara, hospital na miradi mingine inayosimamiwa nana serekali.