Tumbatu FM

Watoto wenye ulemavu wana haki ya kupatiwa elimu

4 June 2026, 13:31

Nipicha inayowaonesha wanafunzi wakiwa maeneo ya shule (Picha na Vuai Juma)

“Ikiwa fursa ya kujifunza itatolewa kwa makundi yote ndani ya jamii kutawezesha watoto wenye mahitaji maalum kufikia malengo yao”

Na Vuai Juma.

Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wameiomba serikali na wadau wa elimu kuhakikisha wanatekeleza sera ya elimu na kuwashirikisha watu wenye ulemu katika sekta hiyo ilikuweza kupata haki hiyo ya kimsingi.

Wakizungumza na Radio Tumbatu FM wamesema kuwepo kwa elimu mjumuisho katika jamii kunatoa fursa sawa ya upatikanaji wa elimu bila ya ubagu hivyo ni vyema kukawekwa mikakati Madhubuti ya kuhakikisha elimu inapatikana kwa watu wote.

Wamesema mbali na muamko wa jamii uliopo wa kuwapeleka watoto wenye ulemavu kwenye taasisi za kielimu zilizopo nchini bado kunautekelezwaji mdogo wa sera za elimu jambo ambalo linadumaza maendeleo ya kielimu kwa Kundi hilo hivyo wameomba utekelezaji madhubuti wa sera na sheria za elimu sambamba na kuweka miundombinu rafiki itakayoweza kuwasaidia.

Kwaupande wake Afisa watu wenye ulemavu wilaya ya Kaskazini “B”  Unguja Abdallah Yahya amekiri kuwepo kwa changamoto zinazo wakumba watu wenye ulemavu kwenye elimu ikiwemo ukosefu wa vyoo kwaajili ya watu hao vifaa vya kufundishia uhaba wa walimu wenye taaluma ya kusimamia watoto wenye ulemavu pamoja na upungufu wa madarsa ya kusomea.

Nae mwenyekiti wa jumiya ya watu wasioona Kaskazini Unguja bi Fatma Mngwali Khamisi ameiomba serikali kuzitatua changamoto zote  zinazowakabili watu wenye ulemavu ili kuboresha upatikanaji wa elimu ndani ya Skuli zao.

Zaidi ya Skuli 10 za Mkoa wa Kaskazini Unguja zinawanafunzi wenye ulemavu zikiwemo Misufini KitopeTumbatu Mahonda Jongowe Kidoti Mapinduzi Mkataleni   na majenzi.