Tumbatu FM
Tumbatu FM
22 June 2026, 10:28

“Tumeona ni vyema kuwafanyia vipimo wasafiri wote wanaoingia Zanzibar kupitia Bandari na Viwanja vya Ndege kwa lengo la kuhakikisha maradhi hayo hayaingii hapa kwetu”
Na Juma Haji.
Wizara ya Afya Zanzibar imesema itaweka utaratibu wa kuwafanyia vipimo watu wote wanaoingia Zanzibar na kutoa miongozo ya matibatu kwa wale watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.
Akitoa ufafanuzi wa maswala yaliyoulizwa na washiriki wa mkutano wa kuwaelimisha viongozi wa jamii na waandishi wa Habari uliofanyika katika kituo cha walimu Bububu Wilaya ya magharibi “A” Unguja afisa kutoka kitengo cha ufuatiliaji wa maradhi Zanzibar (ZEDSU) Dr. Samira Suleiman Khamis amesema Wizara itaweka maafisa wa vipimo kwenye maeneo ya bandari na viwanja wa ndege ili kuhakikisha watu wote wanaoingia Zanzibar wanafanyiwa vipimo kama ilivyo kwa maradhi ya malaria.
Amesema zoezi hilo litakuwa endelevu kutokana na muingiliano uliopo wa wananchi na wageni wanaokuja kutoka nchi jirani ikiwemo Kongo na Uganda kwa shughuli za biashara ambako wagonjwa wa ugonjwa huo wameaza kugundulika.
Akieleza baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Afya Zabzibar katika maandalizi ya kuikinga Nchi na ungonjwa wa Ebola afisa kutoka kitengo cha udhibiti na kupambana na maradhi ya mripuko Zanzibar Dr. Turki Suleiman Ali amesema hadi sasa Wizara inaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa Dini Masheha na wafanya Biashara kutoka kongo na Uganda huku wa wakiwashauri kupunguza safari kibiashara ili kuondoa uwezekano wa kuenea kwa maradhi.
Wakizungumza kwa niaba ya washiriki wa mkutano huo Bw Makame Juma Sheha na Bibi Nachum Shaka Ali kutoka shehia ya kizimkazi mkunguni wameishari Wizara kuendelea na kutoa elimu kwa wananchi pamoja na manahoza wa vyombo vya baharini ili waweze kuwa na muamko wa kupima afya zao wanaporudi kwenye madago.