Tumbatu FM
Tumbatu FM
11 August 2026, 17:05

“Serikali zote mbili zimeweka nazingira mazuri kwa makundi ya vijana hivyo ni vyema kuzitumia ipasavyo ili muwezenkujikwamua na hali ngumu ya kimaisha“
Na Maulid Juma na Mwanahawa Hassan.
Katibu tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Ameir Ali Haji amewahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii katika kuzikimbilia fursa ziliopo ili kujikomboa kiuchumi na kupata maendeleo.
meyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na makundi mbalmbali ya vijana wa Mkoa wa Kaskazin Unguja katika kongamano la vijana ikiwa ni shamra shamra za kuelekea siku ya vijana duniani huko Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini” A” Unguja.
Amesema kongamano hilo limelenga kuwaunganisha vijana katika kutoa changamoto zao na kutoa ushauri kwa serikali huku akisema dhamira kuu ni kuhakikisha uelewa unaongezeka na kuwafanya vijana kuzitumia fursa zilizopo.
Hata hivyo amesema vijana ndio chemchem ya kuibua watendaji wazuri kwenye serikali na kuchochehea ujengwaji wa jamii iliyobora huku akitoa witokwa vijana kujenga utamaduni mzuri na kuepuka vitendo vibaya na hatarishi ambavyo havikubaliki katika jamii.
Kwa upande wake ndugu Abdul- hamid Thabit Mzee kutoka wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEA) amesema kwa mujibu wa shirika la Intergret Labour of servey takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2021 asilimia 27.6% ya vijana wa Zanzibar walionekana kuwa hawana ajira huku takwimu za mwaka 2025 zikionesha kupungua kwa tatizo hilo kwa asilimia 5.4 huku akisema kuwa wamechukuwa jukumu la kuwapatia mafunzo vijana hao juu ya namna ya kuzifikia fursa ziliopo ili waweze kuajiriwa au kujiajiri na kupata mafanikio.
Awali akisoma risala kwa niaba ya vija wa Kaskazini Unguja Naila Bakari Foum amesema licha ya kuwa serikali na taasisi mabalimabli za kiraia zinachukuwa juhudi mabalimbali za kuwajengea uwezo vijana juu ya kuchangamkia fursa ili kujikwamua na umaskin bado Kundi hilo linakabiliwa na changamoto za ucheleweshwaji wa mikopo ukosefu wa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha kutokuwepo kwa masoko ya uhakika pamojana vikwanzo vinavyoathiri watu wenye ulemavu.
Nao baadhi vijana walioshiriki kongamano hilo wamewaomba vijana wengine kuzikimbilia fursa mbali mbali za kiuchumi zilizopo pamoja na kuwa na moyo wa kujitolea na kuacha tabia ya kusubiri ajira kutoka serikalini pekee.
Kongamano hilo limeandaliwa na Jumuia ya Vijana na Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja(JUVIEKA) kwa kushirikiana na shiriika la ActionAid ambapo kilele cha maadhimisho hayo hufanyika kila ifikapo tarehe 12 Agosti 2026 na kwa mwaka huu Visiwani Zanzibar yatafanyika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa ndege.