Tumbatu FM

Watumbatu wahimizwa kusajili matukio ya kijamii

11 August 2026, 21:55

Picha ya wanachi wa kisiwa cha Tumbatu wakiwa katika zoezi la kusajiliwa matukio mbali mbali ya kijamii lililofanyika Akuli ya sekondari Tumbatu wakati maadhimisho ya siku ya usajili barani Afrika (Picha na Juma Haji)

“Nilazima mujenge utamaduni wa kusajili matukio yenu ili kuisadia serikali kuweza kupamga mipingo yake vizuri na kufikia maendeleo ya kweli”

Na Juma Haji

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wananchi kulipa umuhimu swala la usajili wa matukio muhimu ya kijamii ili kufanikisha malengo ya serikali ya kuwa na kumbu kumbu za matukio hayo katika kukuza mipango ya maendeleo ya Nchi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya usajili barani Afrika yaliyofanyika ambapo kwa Zanzibar yamefanyika Wilaya ndogoTumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar Makame Mussa Mwadini  amesema usajili wa matukio utawawezesha wananchi kutambulika kisheria pamoja na kuipa uwezo serekali wa Kupata takwimu sahihi zitakazowawezeka kupanga mgawanyo wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu.

Sauti ya Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa matukio ya kijamii Zanzibar Makame Mussa Mwadini.

Amesema serikali Inaendelea na mkakati wake wa Kusogeza huduma Za matukio ya kijamii karibu na wananchi kwa kutumia mifumo ya kidijitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wakati.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliopatiwa huduma hizo ndugu Haji Abdalla Ali amesema kusogezwa kwa huduma hizo karibu na makaazi ya watu kumewapunguzia wananchi usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuatilia huduma hizo

Aidha ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kuendelea a utaratibu huo mara kwa mara ili wananchi waendelee kupata huduma kwa urahisi.

Katika maadhimisho hayo wananchi wa kisiwa cha Tumbatu wamepatiwa huduma zote za usajili wamatukio ikiwemo Vizazi hai na Vifo pamoja na vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi.