Tumbatu FM
Tumbatu FM
21 June 2026, 17:07

“ikiwa jamii itaacha tabia ya kuharibu mazingira kwa kukata miti kiholela kutasaidia kuongozeka kwa samaki katika bahari hivyo ni vyema kuyatunza mazingira kwa faida ya nchi kwa ujumla”
Na Atka Mosi Makame
Wananchi wametakiwa kuhifadhi misitu kwa kuazisha kamati za usimamizi wa misitu ndani ya shehia (COFMA) zitakazo weza kusimamia mali asili na rasilimali za misitu na Bahari.
Hayo yameelezwa na mtaalam wa idara ya misitu katika hifadhi ya taifa Jozani Aziza yunus Nchimbi wakati akifungua mafunzo ya siku kuhusu utunzaji wa mazingira yaliyoaandaliwa na jumuiya ya Vijana na elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja JUVIEKA katika ukumbi wa walimu (TC) Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema kamati hizo zipo kisheria kwa mujibu wa sheria namba 10 kifungu cha 36 na 47 ambapo zitakua zinashirikiana na idara ya misitu na kupewa mikataba ya kiserikali ili kulinda rasilimali za asaili hapa Zanzibar.
Hatahivyo amesema Baahari ya Zanzibar imekua na changamoto nyingi kutokana na uharibufu wa mistu jambo linalopelekea kutokea upungufu wa Samaki hivyo ipo haja kwa jamii kueendelea kupatiwa elimu ya kutuza rasilimali asili na utuzaji wa mazingira kwenye misitu na Bahari ili kuepukana na changamoto hiyo.
Aidha amefahamisha Kuwa kutofuata taratibu za uvuvi zinazotolewa na wataalam nako kunachangia kukosekana kwa zao la Samakihuku akiwataka wanajamii waliopatiwa mafunzo hayo kui fikisha elimu hiyo kwa wengine ili kuacha tabia ya kutupa taka na ukataji mikoko kiholela.
Mkurugezi wa jumuiya ya vijana na elimu Kaskazin Unguja (JUVIEKA) Mabrouki Maalum amesema lengo la mafuzo hayo ni kuwafahamisha wahusika wa kamati hizo juu yanamna ya kutuza rasilimali asili na baianuwai zilizowazunguka kwa ustawi wa jamii.
Amebainisha kuwa wameweka mikakati mbali mbali ya kuisaidia jamii ikiwemo kushirikisha makundi yote ya wana jamii serikali na asasi za kiraia ili kutafuta rasilimali zitakazo tatua changamoto kwa kupatikana vitendea kazi vitakavyo saidia kupunguza uchafuzi wa mazira.
Kwaupande wake afisia misitu kutoka Wilaya ya kaskazin “A” Sleyum Saidi amesema elimu hiyo wameipokea vizuri na kuahidi kuyafanyia kazi yote waliojifuza huku wakisema hatua zitachukuliwa kwa atakeenda kinyume na taratibu zilizopo.
Nao walishiriki wa mafuzo hayo wamesema wamefurahishwa nataaluma waliyopatiwa na kuahidi kutoa mashirikiano ili kuleta maendeleo ya hifadhi ya misitu.
Ni washiriki kutoka kamati za usimamizi wa misitu (COFMA) wakiwa kwenye mafunzo kuhusu utunzaji wa mazingira.