Tumbatu FM
Tumbatu FM
6 May 2026, 10:12

“Ikiwa mnahitaji kupata maendelo nilazima viongozi mkubali kuwashirikisha wananchi kutoka kwenye makundi yote ndani ya jamii bila ya ubaguzi.
Na Vuai juma.
Viongozi wa Wilaya Kaskazini “B” Unguja wametakiwa kuwajibika katika majukumu yao sambamba na kuwashirikisha wananchi wakati wa kufanya maamuzi.
Wito huo umetolewa na katibu tawala wa Wilaya hiyo Hassan Abdallah Rashid wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa viongozi wa shehia vijana wanawake na watu wenye ulemavu ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mradi wa uwezeshaji wa jamii kwa ajili ya haki za binadamu na utawala bora unaosimamiwa na idara ya maendeleo ya jamii kanisa katoliki jimbo la Zanzibar yaliyofanyika Skuli ya Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema maamuzi mazuru na halisi ambayo yanalenga kufikia maendeleo ya kweli yanatakiwa yatoke ngazi ya chini hivyo ni vyema viongozi kuacha tabia ya kufanya mambo kwa matakwa yao binafsi badala yake wawashirikishe wanchi kutoka kwenye makundi yote.
Aidha amezitaka Taasisi nyengine kutafuta wafadhili watakao wawezesha kuandaa na kutekeleza miradi ya kimaendeleo itakayoweza kuisaidia serikali katika utowaji wa huduma mbali mbali ndani ya nchi.

Awali Afisa tathimini na ufuatiliaji Idara ya maendeleo kanisa katolik Zanzibar Msafiri Thomas Mombo amesema moja ya malengo ya mradi huo ni kujenga mazingira wezeshi ya upatikanaji wa ardhi elimu bora na fursa endelevu za masuala ya kiuchumi huku akisema wanategemea kukuza ushiriki wa watu wenye ulemavu vija na wanawake ndani ya kamati zitakazoundwa katika shehia zao.
Kwaupande wake mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa jamii kwaajili ya haki za binadamu na utawala bora kutoka idara ya jamii kanisa katoliki jimbo la Zanzibar Sister Editha Simwe amesema wameandaa mafunzo hayo ili kuhakikisha wanajamii na viongozi wanatambua umuhimu wa utawala bora na namna ya kufanya maamuzi shirikishi yatakayowaweka pamoja wakati wa kutekeleza shuhuli zao.

“Tumeyapokea kwa vizuri mafunzo haya taaluma hii ambayo tumepatiwa itatusaidia sana na tutaifanyia kazi kwa vitendo kwa manufaa ya makundi tunayowakilisha”
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema wameipokea vizuri elimu waliyopatiwa ambayo imewapa matumaini mapya huku wakiahidi kuichuku na kuwafikishia wengine kwa lengo la kuifanyia kazi kwa Pamoja.
Mradi wa uwezeshaji wa jamii kwa ajili ya haki za binadamu na utawala bora unasimamiwa na idara ya maendeleo ya jamii kanisa katoliki jimbo la Zanzibar kwa ufadhili wa Misereo naunatekelezwa ndani shehia tano za wilaya ya Kaskazini “B” Unguja ambazo ni Mkataleni Mahonda Kitope Misufini na majenzi.