Tumbatu FM
Tumbatu FM
22 June 2026, 11:42

“Fikisheni elimu hii kwa watu mnaowaongoza ndani ya jamii nyinyi ni nguzo muhimu kwenye mapambano dhidi ya upotevu wa uoto wa asili ambao unazidi kutoweka”
Na Atka Mosi Makame.
Mkurugezi wa jumuiya ya vijana na elimu Mkoa wa kaskazini Unguja Mabrouk Maalum Mohamed amewataka masheha walimu wakuu wa skuli na wenyeviti wa kamati za skuli kutuza mazingira yanayowazunguka na kufikisha elimu kwa jamii ili kuepukana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Ameyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa mafuzo kuhusu mazingira yaliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu TC Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini unguja.
Amesema mabadiliko ya tabia nchi yanatokana na hali ya hewa ya muda mrefu yanasababishwa na uchafuzi wa mazingira kwa ukataji miti,uchimbaji mchanga hali ambayo inapelekea kuengezeka kwa joto.
Amesema lengo la mafuzo hayo ni kutafuta namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi hususan katika jamii na mazingira ya skuli huku akisema kuwa washiriki hao wana nafasi kubwa ya kuchangia mabadiliko na kueneza elimu hiyo kwa jamii husika jambo ambalo litasaidia muonekano mzuri na wenye haiba ya kuvutia
Hata hivyo amesema Zanzibar imeanza kushuhudia Athari za mabadiliko ya tabia nchi jambo linalopelekea kuongezekakwa kina chamabji ya Bahari huku akitowa wito kwa serikali na wanajamii kuendeleza kudumisha utunzaji wa mazingira.
Baadhi ya masheha waliopatiwa mafunzo hayo wameipongeza jumuiya ya JUVIEKA kwa kuwapatia elimu hiyo na kuahidi kuifanyia kazi kwa kuelimisha watu walio wazunguka kuhusu madhara ya uharibifu wa mazingira na kuwashajihisha ujuu ya umuhimu wa upandaji miti.
Akizungumza kwa niaba ya wawakilishi kutoka skuli zilizoshiriki mkutano huo mwalim Bakari Ali kutoka shule ya Mapinduzi sekondari chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja amesema elimu hiyo imekuja wakati muwafaka na watahakikisha wanaifikisha kwa wanafuzi na wazazi ili kuimarisha uwelewa wa haraka.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wwameshukuru kupatiwa elimu hiyo na kusema watajitoa katika kuifikisha kwa jamii na kutoa wito kwa vijana kuacha kujitengenezea ajira zinazotokana na uharibifu wa mazingira.
Mafuzo hayo yasiku Mbili yamesimamiwa na jumuia ya Vijana na elimu Mkoa wa kaskazini Unguja (JUVIEKA) kwa ufadhili wa ActionAid ambapo yaliyowashirikisha masheha wenyeviti wa kamati za Skuli Maafsa Misitu na Walimu wa kuu.