Tumbatu FM
Tumbatu FM
8 August 2026, 15:38

“Uwepo wa mashirikiano kati ya masheha kamati za shehia na wananchi ni jambo la muhimu katika kufikia malengo yenu mliyojiwekea nivyema ukamngana pamoja ili mupate mafanikio”
Na Mwanahawa Hassan
Mkurugenzi wa jumuia ya vijana Elimu Mkoa wa Kaskazini unguja ( JUVIEKA) Mbarouku Maalum Mohamed ambae pia msimamizi wa mafunzo katika mradi wa IMARISHA FAMILIA unaotekelezwa na shirika la SOS Zanzibar ameutaka uongozi wa shehia ya Jongowe kushirikiana na wanajamii katika kutekeleza mpango kazi wa maendeleo ya shehia hiyo.
Ameeleza hayo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokoton Wilaya ya Kaskazin “A” Unguja mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuaandaa mpango kazi wa maendeleo ya jamii utakaowasaidia katika kutekeleza majukumu yao ili kupata maendeleo.
Amesema mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa wananchi hao kwani umeweza kubainisha rasilimali walizonazo na kuonyesha changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii yao jambo ambalo amelitaja kuwa ni hatua muhimu ya kuweza kujua namna ya kutekeleza mradi huo.
Aidha amewataka wanufaika wa mafunzo hayo kuwa tayari katika kuzisimamia changamoto walizo zibainisha ili kuona namna gani wanaweza kuzitatua.
Kwaupande wake Ndugu Othman Hadhir Othman ambae ni miongoni mwawashiriki wa mafunzo hao amesema amefurahishwa na elimu waliyopatiwa kutokana na umuhimu wake kwani itaweza kuwasaidia wakati wa kutekeleza mpangokazi huo na kupata matokeo mazuri.
Mafunzo hayo ya siku Tatu (3) yametolewa kwa wakazi wapatao 15 kutoka shehia ya Jongowe Pamoja na maafisa mbali mbali wa Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja kwa ufadhili wa shirika la SOS Zanzibar.