Tumbatu FM

Uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja yazindua kampeni ya Mjue jirani yako

19 November 2026, 21:36

Picha ya wananchi wa Bumbwini Misufini, Wilaya ya kaskazini B Unguja wakisikiliza maelezo ya maafisa Uhamiaaji, Picha na Juma Haji

“kila mwananchi awajibike kutoa taarifa za uhalifu pale anapoona matukio ya uhalifu ili vyoombo vya ulinzi viweze kufuatilia na kuchukua hatua zinazofaa kishehia“

Na Juma Haji

Wananchi wa Mkoa wa kaskazini Unguja wamehimizwa kuviunga mkono vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za watu wasiowajua ili kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii zao.

Wito huo umetolewa na mrakibu msaidizi wa uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja Haji Soud Mzee huko Bumbwini misufini Wilaya ya kaskaini “B’ Unguja  katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya mjue jirani yako inayoendeshwa na Ofisi ya uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja.

Haji amesema ili kazi ya kulinda nchi na mipaka yake iwe rahisi ni vyema kila mwananchi kuwa na uzalendo wa kutoa taarifa za watu asiowajua pamoja na viashiria vya matukio ya kihalifu ili vyombo  vya ulinzi na usalama ikiwemo Uhamiaji viweze kufuatilia na kudhibiti matendo hayo.

Akitaja makosa ya uhamiaji haram Mrakibu Haji  amesema Sheria ya Uhamiaji Na. 7 ya mwaka 1995, Sura ya 54, Kifungu cha 47,ina mamlaka ya kumtia hatiani mtu yoyote atakaemsaidia au kumuhifadhi muhamiaji haram aliyeingia nchini kinyume na sheria za nchi.

Sauti ya mrakibu msaidizi wa uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja Haji Soud Mzee.

Amesema wananchi hasa masheha wa na wajibu wa kufuatilia mienendo ya kila raia aliyepo kwenye shehia ili kujua uhalali wake kwani wapo raia katika baadhi vijiji baada ya kuishi kwa muda mrefu sheria imewapa nafasi ya kuomba uraia na sasa ni raia wa zanzibar.

katika picha hii anaonekana mrakibu msaidizi wa uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja Haji Soud Mzee, aliesimama

Akiwasilisha maada Afisa tehama kutoaka Ofisia ya Uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja Mwinyichande Othman Ali amesema wameamua kutumia njia rahisi ya kutoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha kila mwananchi anapata uelewa wa kampeni ya mjue jirani yako na anatoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya usalama ili kulinda kasi ya uhamiaji haram katika maeneo mbali mbali ya shehia za Mkoa wa kaskazini Unguja.

Amesema mfumo uliopo kwa sasa wa kimtandao unamruhusi mwananchi kuanza taratibu za kuomba huduma zinazotolewa na Ofisi hiyo ikiwemo visa na uraia na wanaweza kufika Ofisini kwa hatua za wmisho kukamilisha mchakato wa maombi

Picha ya Mwinyichande Othman Ali aliesimama hapo mbele kuwasilisha maaada ya matumizi ya mitandao katika kufuatilia huduma zinaotolewa na Ofisi ya uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja, na Picha Nishan Khamis

Nao wananchi walioshiriki mkutano huo akiwemo Bi Hawa Rashid Seif na Bw Abrahman Sulaiman Ali na  na wameisifu Ofisi ya uhamiaji Mkoa wa kaskazini Unguja kwa kazi kubwa wanayoifanya katika majukumu yao ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi kwa kufika kwenye maeneo yao na kuahidi kuifikisha elimu hivyo kwa wananchi wengine.

Sautia za baadhi ya wananchi wakitoa maoni yao mara baada ya kupatiwa elimu ya uraia kupitia campeni ya Mjue jirani wako.