Tumbatu FM
Tumbatu FM
14 October 2026, 09:53

Picha ya Mstaiki meya wa manispa kaskazini “A’ Unguja Mhe Nyange Kheri Ali , Picha na Atka Mosi Makame
“Kwa wezetu manispa za wenzetu zimetuzidi sana ukilinganisha na manispa za kwetu Zanzibar” kauli yake Mhe Nyange Mstaiki meya wa Manispa kaskazini “A’ Unguja akiwa kwenye kipindi Radio jamii Tumbatu
Na Mwanahawa Hasan
Imeelezwa kuwa moja ya njia rahisi kwenye uongozi ni ile ya kujifuza tabia na mifumo ya maisha ya watu, njia hii humpa nafasi mtu wa kawaida au kiongozi kujua tabia nzuri na maya za mshindani wake au mtu aliepitia shughuli/che au nafasi kama ya kwake.
Hayo yamebainika kwa Mhe Nyange Kheri Ali aliposhiriki kipindi maalum cha “Yafanywayo na viongozi” kinachosimamiwa na Tumbatu FM chenye lengo la kuwapa nafasi viongozi kuelezea mambo wanayoyafanya na yanayowakuta katika safari yao ya uongozi
Makala hii itakupa picha halisi ya jinsi Madiwani na viongozi wengine wa kaskazini Unguja walivyosafiri hadi jijini Dodoma pamoja na kukuonesha mafanikio waliyoyapata ambapo kimsingi ni juhusi zao za kuwaletea wananchi maendeleo wakiamini kuwa safari hiyo itabadilisha mwelekeo wa Manispa hii na kufannana na Manicpa nyengine zilizopo hapa zanzibar zilizo mbele kimaendeleo.