Tumbatu FM

Je, mtoto wa kiume huandaliwa kutekeleza shughuli za nyumbani?

23 November 2026, 13:36

Wanaoonekana hapo ni baadhi ya wakazi wa shehia za Mkokotoni, Mtoapwani na Pale Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakifuatilia mafunzo ya jinsia.

“Kugawa majukumu kati ya watoto wa kike na wa kiume ni jinsi ya kuwa hubagui kama wanawake wanapaswa kufanya majukumu fulani tofauti na wanaume”

Na Mwanahawa Hassan Khamis

Wazazi na walezi nchini wametakuwa kutoa fursa sawa kwa watoto wao ili kuwajenga katika malezi bora na kuwa na misingi imara ya kundeleza familia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkufunzi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar Ndg: Muhamed Jabir wakati akizungumza na Tumbatu FM  mara baada ya kukamilika mafunzo ya jinsia yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano skuli ya sekondari ya Mkokotoni Wilaya ya kaskazini”A” Unguja. 

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wazazi na walezi wa Mkoa wa kaskazini Unguja juu ya dhana ya mgawanyo wa majukumu katika familia kwa watoto bila ya kuangalia jinsia.

Amesema mfumo wa maisha uliopo si wakutegemea majukumu hasa ya nyumbani kukamilishwa na watoto wa kike pekee badala yake kujenga utamaduni wa kuwashirikisha watoto wa kiume kwenye majukumu hayo ili na wao wapate mazowea ya kufanya shughuli za nyumbani na katika mazingira yanayozunguuka familia.

Aidha, amesema amefurahishwa na wananchi wa shehia zilizoshiriki mafunzo hayo kwa kushrikiki kupanga mipangokazi ambayo itawaongoza katika kuendeleza masomgo waliojifunza.

Sauti ya Mkufunzi wa mafunzo Ndg: Muhamed Jabir

Kwa upande wao washiriki  wa mafunzo hayo wamesema wanaishukuru taasisi ya JUVIEKA kwa kuwapatia mafunzo yatawasaidia utekelezaji wa  mpango kazi waliyoitaarisha na ambayo wataitumia kwenye kaya zao na kupata maendeleo na ustawi wa familia.

Sauti ya baadhi ya wanajamii walioshiriki mafunzo hayo.

Mafunzo hayosiku tatu yameandaliwa na juvieka kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society na yamezishirikisha shehia tatu za Wilaya ya kasakazini A Unguja shehia ya Mkokotoni, Mtoapwani na Pale.