Tumbatu FM

Waislam wahimizwa kuanza maandalizi ya ibada ya Hijja

28 September 2026, 16:45

Pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hijja ya Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (UTAHIZA) Shekh Mohamed Mansour Mohamed akitoa taarifa ya maandalizi ya Hijja. Picha na Juma Haji

Iwapo mahujaji wataanza maandalizi ya ibada ya Hijja mapema ni rahisi kuchagua taasisi yenye vigezo na huduma nzuri.

Na Juma Haji

Waislam wenye nia ya kushiriki ibada ya hijja kwa hijja ya mwaka 2027 sawa na mwaka 1448 hijiriya wametakiwa kuanza kujiandikisha mapema ili kupata muda wa kutosha wa kushiriki kila hatua ya maandalizi ya ibada hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari uko katika ukumbi wa Masjid Nur-Muhamad uliopo kwa mchina mwazo, Wilaya ya magharibi “B” Unguja mwenyekiti wa kamati ya hijja ya umoja wa taasisi za hijja Zanzibar (utahiza) Shekh Mohamed Mansour Mohamed amesema kufanya maandalizi mapema kunaziwezesha taasisi za Hijja kutatua changamoto za mahujjaji mapema kabla ya muda wa mataarisho kuisha.

Amesema utahiza kwa upande wake ilianza maandalizi baada ya kukamilika kwa ibada ya hijja ya mwaka jana kwa kuzisimamia taasisi zilizochini yake kuondoa mapungufu yaliyojitokeza na  kuboresha hubuma bora zao.

Akizungumzia maandalizi kwa hija ya mwaka 2027 Shekh Mohamed amewataka waislam kuanza kujiandikisha huku akisema kuwa kujiandikisha ni hatua ya awal na hujajaji baada ya kujiandikisha ataendelea na hatua nyengine kulingana na miongozo taasisi aliyoichagua.

Sauti ya mwenyektiki wa UTAHIZA wakati akizungumza.

Wakiuliza maswali Baadhi ya waandish wa habari walioshiriki mkutano huo Akiwemo Bw Khatibu Slaiman wa gazeti la Habari leo na Bibi Rahma Sulaiman wa Garzet la Nipashe wameipongza taasisi ya utahiza kuzisimamia vyema taasisi zake katika kutimiza lengo la hijja kwa mahujaji.

Jumla ya taasisi 25 zimekidhi vigezo vya kushafirisha mahujjaji mwaka huu kati ya taasisi 35 zinazojishughulisha na kazi ya usafirishaji mahujajji Zanzibar.