Tumbatu FM

Juvieka na Institute of Excellence Knowledge zawazawadia wanafunzi wao

29 November 2026, 08:40

Pichani ni wanafunzi wa Taasisi ya Institute of Excellence Knowledge (IEK) na viongozi wa Juvieka wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la zawadi kukamilika, Na picha Juma Haji

Iwapo walimu wataongeza kasi na mbinu za ufundishaji watasaidia kukamilika kwa lengo la serekali la kuandaa kizazi chenye uelewa na uwezo katika kutimiza dira ya malengo ya maendeleo ya taifa kielimu kuelekea Dira ya 2050.

Na Juma Haji.

Jumuiya ya vijana na Elimu kaskazini Unguja JUVIEKA imesisitiza umuhimu wa uwekezaji katika elimu kama msingi wa kujenga jamii yenye maarifa na kuongeza ufaulu wa masomo kwa wananfunzi

Akikabidhi zawadi kwa wanafunzi mbali mbali katika maadhimisho ya miaka mitatu ya Taasisi ya Institute of Excellence Knowledge (IEK), huko Skuli ya Secondary Mfenesini, Shehia ya Vuga mkadini, Mkoa wa Mjini Mgharibi Unguja Afisa Habari wa Jumuiya Vijana na Elimu kaskazini Unguja Ndugu Mohamed Juma amesema iwapo wanafunzi watakomaa kielimu na uwezo wa kufikiri utaongezeka na hivyo kurahisissha kufaulu masomo yao.

Aidha, amebainisha kuwa juhudi hizo zina mchango mkubwa katika utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi katika kukuza uwajibikaji na kuwekeza nguvu zaidi katika sekta ya elimu na maeneo mengine.

Amesema JUVIEKA inaamini kuwa elimu si darasa pekee, bali ni uwekezaji wa maarifa ndio unaojenga jamii, kufungua fursa na kuandaa viongozi wa kesho.

Taasisi ya Institute of Excellence Knowledge (IEK), inachangia kupanua fursa za elimu kupitia mafunzo ya kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watu wazima, watoto na vijana imeingia katika historia ya taasisi zinazoekeza kwenye elimu ndani ya Mkoa wa Mjini Magharini