Tumbatu FM

Data za tajwa kuongeza kasi ya utatuzi wa tatizo la ajira kwa vijana Zanzibar

23 November 2026, 16:56

Wa kwaza upande wa kulia ni Bi Salama Mbarouk Khatibu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji,SMZ , Na picha Sauda Silima Khamis- Wizara ya kazi, Ajira.

Mpango wa kuwafikia vijana 37.3% Visiwani Zanzibar ukikamilika utazidi kuongeza kasi ya ongezeko la vijana wasio na ajra.

Na Sauda Silima Khamis- Wizara ya kazi, Ajira, Vijana na uwezeshaji Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji, Salama Mbarouk Khatibu, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mikakati ya kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii kwa kuwapatia elimu na maarifa yatakayowaongezea uwezo wa kuendesha miradi yao na kujitegemea.

Ameyasema hayo alipokutana na watendaji wa taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na Wizara hiyo pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), kupitia mradi wa SYP, katika Ofisi za Wizara hiyo Magomeni Wandaras, Wilaya ya Mjini, Unguja.

Amesema kijana kupatiwa elimu ya afya, uchumi na teknolojia ni jambo muhimu ambalo humuwezesha kujitambua na kutambua fursa zilizopo katika mazingira yake pamoja na kutumia maarifa aliyoyapata kujiendeleza na kujitegemea.

Ameeleza kuwa Serikali imebeba dhamana ya kuhakikisha vijana wanapata mazingira bora, elimu na ujuzi utakaowawezesha kufikia malengo yao na kujikwamua kiuchumi, kama inavyoelekezwa katika Sera ya Maendeleo ya Vijana.

Amesema serekali itazidi kuandaa mazigira mazuri kwa kuwatambua vijana waliomaliza masomoili iki waweze kuajirika kupitia serekali na taasisi nyengine zenye uhitaji wa wataalam.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji, Salama Mbarouk Khatibu.

Amesema kufanikiwa kwa mkakati huo vijana wengi wataweza kuelekeza nguvu zao katika shughuli za maendeleo na kujiepusha na vitendo visivyofaa katika jamii.

Amesema mkakati huo pia utaenda sambamba na malengo ya serekali kupitia Wizara Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji ya kuhakikisha wizara inawafikia 37.3% ya vijana, kundi lenye watu wengi wenye uhitaji wa shughuli za kazi hapa visiwani Zanzibar.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji, Salama Mbarouk Khatibu,

Kwa upande wake, Msimamizi wa UNFPA Zanzibar, Maryam Naeje, alisema amefurahishwa na ushirikiano wanaoupata kutoka Wizara hiyo, akieleza kuwa lengo la ziara yao ni kujifunza na kujionea namna vijana waliopatiwa mafunzo kupitia mradi wa SYP wanavyotumia elimu hiyo katika shughuli zao.

Aliyesimama kati na kati ni Msimamizi wa Shirika la UNFPA Zanzibar Bi Maryam Naeje.

Amesema ziara hiyo pia imelenga kufahamu iwapo vijana waliopatiwa mafunzo wameweza kuyafanyia kazi maarifa hayo na kuyasambaza kwa vijana wengine katika maeneo yao.

Ujumbe wa UNFPA umesema kupitia ziara hiyo umejifunza namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyoandaa mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujiendeleza na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Ujumbe huo umeahidi kuendelea kuangalia na kutambua vipaumbele vya vijana wa Zanzibar ili mipango kazi ya shirika hilo iendane na mahitaji yao na kuwawezesha kuimarisha miradi wanayoisimamia