Tumbatu FM
Tumbatu FM
4 October 2026, 20:05

Aliesimama mbele ni katibu tawala Wilaya ya kaskazini “A”Unguja wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo. na picha Juma Haji
“Maandaalizi kwa wanaojiandaa kuhama kupisha mvua ya El-nino yahusishe kutambua maeneo yaliyo salama kuishi na kuwa na akiba ya kutafuta huduma wakati wa majanga”.
Na Juma Haji Juma
Wananchi waliopo maeneo yanayotabiriwa kuathirika na mvua za El-nino wameshauriwa kufanya utafiti wa maeneo wanayotegemea kuhamia kupisha mvua hizo ili kujiepusha kadhia ya kuhama hama.
Akifunga mafuzo ya siku moja yaliyoandaliwa na jumuiya ya elimu na vijana kaskazini Unguja JUVIEKA kwa ushirikiano na Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya kaskazini ” Unguja ”katibu Tawala Wilaya ya kaskazini A” Ndugu Farid Mohanned Haji amesema wananchi kuwa na taarifa za sehemu wanazohamia kabla ya kuhamia itawapa uhakika wa kujua usalama wa maeneo hayo na kuwa na uwezo wa kukabiliana na athar za mvua zinazotabiriwa kutokea.
Amewataka wanchi kuweka akiba za vyakula ili viwasaidie pale majanga yatakapowakuta wakati ambao ni vigumu kufanya kazi na kujipatia kipato.
Sauti ya katibu tawala Wilaya ya kaskazini A” Ndugu Farid Mohanned Haji
Akiwasilisha maada katika mafuzo hayo Afisa maafa wa Wilaya ya kaskazini A” Bi Mosssi Ame Kombo amewataka washiriki mafunzo hayo kwenda kuweka tahadhari za mvua na madhara yake katika jamii zao ili jamii iwe na uwezo wa kukabiliana na majanga hayo pindi yatakapotokea.
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya unyeshaji wa mvua za El-nino za mwaka huu zilizotangazwa na mamlaka ya hali ya kewa Tanzania TMA mvua zinategemewa kuwa kubwa na ambazo hazijapata kutokea kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Amesema kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kuhakiki mapaa ya nyumba zao pamoja na kuhama maeneo yenye kutuwama maji ili kujiepusha na madhara ya majanga ya mvua yasiwakute.

Pocha ya Afisa maafa wa Wilaya ya kaskazini A” Bi Mosssi Ame Kombo ambae ni mkufunzi wa mafuzo hayo
Sauti ya Afisa maafa wa Wilaya ya kaskazini A” Bi Mosssi Ame Kombo
Nae Mkurugenzi wa Jumuiya ya vijana na elimu kaskazini Unguja Mbaruku Maalum Mohamed amewataka wananchi kutodharau tahadhari zinazotolewa na serekali pamoja na wadau wengine. ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Akitoa uzowefu wa athari za mvua kama hizo zilizotokea miaka iliyopita amesema wanachi walisalimika na madhara ya mvua hizo hayo kwa kutii na kufuata maelekezo waliopewa na serekali.
Sauti ya Mkurugeni wa jumuiya ya vijana na elimu kaskazini Unguja Ndugu Mbaruku Maalum Mohamed