Tumbatu FM
Tumbatu FM
2 October 2026, 20:43

Aliesimama mbele ni Mkurugenzi wa jumuiya ya vijana na elimu kaskazini Unguja JUVIEKA Ndugu Mbarouk Maalim Muhammed akiwa katika mafunzo maalum ya kubainisha fursa kwa vijana. Na Picha latifa Ali.
Maendeleo ya vijana yatapatikana kwa urahisi pale watakapofanyakazi ya kuzijua changamoto na fursa na kuzifanyia kazi kwa vitendo.
Na mwandishi wetu Latifa Ali.
Mkurugenzi wa jumuiya ya vijana na elimu kaskazini A JUVIEKA Mbarouk Maalim Muhammed amewataka vijana kutumia fursa mbali mbali za kijamii ili kuibua changamoto pamoja na fursa zilizopo kwenye jamii .
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya harakati za kijamii huko ukumbi wa mikutano Mkwajuni TC Wilaya ya kaskazini A” Mkoa wa kaskazini Unguja .
Amewataka vijana wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo kuchangamkia fursa kwa kujifunza yanayoelekezwa na sera za maendeleo ya jamii pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi.
Amewaasa vijana kutotumia taratibu zisizofaa kwa kisingizio cha kupambania fursa zilizowazunguuka na badala yake wajikite kufatilia miongozo ya sera kuelekea kwenye utatuzi wa changamoto zao
Sauti ya mwenyekiti wa jumuiya ya vijana na elimu kaskazini Unguja wakati akiwasilisha maada kwenye mafunzo hayo.
Nao wanufaika wa mradi huo wamesema kupatiwa mafunzo hayo kumewajengea uwezo na uthubutu katika kutambua maana sera na umuhimu wake katika harakati zao za kimaisha
Sauti ya wanajamii walipana nafasi ya kushiriki mafunzo hayo
Mafunzo hayo ya siku tatu 3 yameandaliwa na Jmuiya ya vijana na elimu kaskazini Unguja JUVIEKA wakishirikiana na shirika la Actionaid pamoja na Global platform yamewakusanya vijana kutoka Wilaya mbali mbali za Unguja.