Tumbatu FM
Tumbatu FM
22 November 2026, 10:16

“Tumekuja kufanya uhakiki huu ili kuweza kufahamu maendeleo ya watoto wetu na kujua namna gani tunaweza kujipanga kwaajili ya kutatua changamoto ambazo tumeziona kwa siku zijazo”
Na Vuai Juma.
Shirika linaloshuhulikia masuala ya elimu kwa wanawake Zanzibar FAWE limefanya ziara maalum kwa wanafunzi wa shehia za Tumbatu Kichangani wanaonufaika na mradi wa kupatiwa vifaa vya Skuli unaofadhiliwa na shirika hilo.
Akizungumza na Tumbatu FM mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo Afisa Programe wa FAWE Zanzibar Tatu Ali Mtumwa amesema lengo la ziara hiyo ni kufanya tathimini ndogo kwa Watoto wenye mazingira magumu waliosaidiwa vifaa vya Skuli ili kuweza kujua namna wanavyoendelea katika masomo yao.
Amesema wamefanikiwa kuweza kugundua mambo mbali mbali ikiwemo changamoto ya watoto wengi kutovitumia baadhi ya vifaa walivyo patiwa ipasavyo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya kielimu kwa wanafunzi hao.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwahamasisha watoto wao kutumia zana walizo patiwa ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa ambayo yanaweza kuwawezesha kuweza kujikomboa kielimu ndani ya familia zao.
Kwaupande wake Sheha awa shehia ya Mtakuja Makame Nyange Juma ambae amezungumza kwa niaba ya masheha wezake amesema wameupokea mpango huo vizuri kutokana na mchango wake mkubwa kwa watoto yatima na wenye mazingira magumu kwani umeweza kuwasaidia sana kupunguza tataizo la uhapa wa vifaa vya kusomea.
Nao baadhi ya wanafunzi walionufaika na mradi huo wametowa shukurani zao kwa taasisi ya FAWE Zanzibar kwa kuweza kuwapatia vifaa hivyo huku wakiahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo samabamba na kuwaomba waendelee kuwasaidia kwa mara nyengne.
Jumla ya wanafunzi 112 wamenufaika na mradi wa kupatiwa vifaa vya Skuli vilivyotolewa na taasisi ya FAWE Zanzibar katoka shehia za Mtakuja Uvivini na Gomani.