Savvy FM

DC Arumeru azindua kituo cha mafunzo kwa walimu kanda ya Kaskazini

14 October 2026, 9:05 am

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Neema Lugangira akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha ufundishaji na mafunzo kwa walimu kanda ya Kaskazini. Picha na Gasper Sambweti.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Neema Kachiki Lugangira, amezindua kituo cha ufundishaji na mafunzo kwa walimu wa Kanda ya Kaskazini katika Shule ya Msingi Naurei, iliyopo kitongoji cha Sokoni Barazani, wilayani Meru.

Na Gasper Sambweti

Akizindua kituo hicho, Bi. Lugangira ameishukuru Vodacom Foundation kwa kufadhili ujenzi wa majengo mawili pamoja na kutoa kompyuta zitakazotumika kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata mafunzo na ujuzi wa teknolojia.

Kituo hicho ni cha kwanza kuzinduliwa katika mpango unaotekelezwa na Vodacom Foundation, huku vituo vingine zaidi ya 50 vikiwa katika hatua za maandalizi ya uzinduzi.

Sauti ya Mkuu wa ilaya ya Arumeru, Bi. Neema Lugangira

Kwa upande wake, Mkurugenzi msaidizi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah amesema kuwa wamefurahishwa na ushirikiano walioupata kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meru, ambayo ilikubali na kutoa nafasi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho katika Shule ya Msingi Naurei.

Mkurugenzi msaidizi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo ametoa shukrani kwa kukabidhiwa kituo hicho, huku akieleza changamoto ya shule hiyo kukosa uzio na kuiomba mamlaka husika kusaidia kutatua changamoto hiyo.

Akihitimisha uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Meru, Bi. Neema Kachiki Lugangira, amewataka wananchi wa kitongoji cha Sokoni Barazani kushirikiana katika kutunza na kulinda mradi huo ili uweze kutoa manufaa yaliyokusudiwa kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla.