Savvy FM
Savvy FM
8 May 2026, 6:56 pm

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini DCEA kanda ya kaskazini imekabidhi vitanda 80 na magodoro 160 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43 kwa waraibu zaidi ya 500 wanaoishi katika nyumba za upataji nafuu mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mazingira ya tiba na urekebishaji.
Na Mariam Mallya
Akikabidhi vifaa hivyo kwa waraibu na wasimamizi wa nyumba za upataji nafuu, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude amewatahadhari kwa vijana watakao jihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema serikali ipo macho na itaendelea kuwa chukulia hatua wale wote wanaojihusisha na biashara hii haramu.
Kwa upande wake, Afisa ustawi wa elimu wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kanda ya Kaskazini Bi. Sarah Ndaba, amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wadau Katika kudhibiti Matumizi ya dawa za kulevya na kuahidi kusimamia vitanda na magodoro hayo ili yadumu na kutumika kama ilivyokusudiwa
Nao baadhi ya waraibu walionufaika na msaada huo wameeleza hisia zao na jinsi jamii inavyowachukulia