Savvy FM

Arusha kuadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 05

3 Machi 2026, 23:13

Mratibu wa jinsia halmashauri ya jiji la Arusha Angelina Christian akizungumza katika studio za Savvy Fm. Picha Mariam Mallya.

Wananchi wa jiji la Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika kimkoa siku ya Machi 05/2026 katika viwanja vya Ngarenaro mkoani Arusha.

Na Mariam Mallya

Akizungumza katika Studio za Savvy FM Mratibu wa jinsia halmashauri ya jiji la Arusha Angelina Christian amesema mkoa huo umejipanga vizuri kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika vizuri nakuwataka wajasiriamali kuleta bidhaa zao ili kujitangaza.

Sauti ya Mratibu wa jinsia halmashauri ya jiji la Arusha Angelina Christian

Aidha Mratibu wa jinsia halmashauri ya jiji la Arusha Angelina Christian amewasihi wanaume kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya wanawake na kusema hakuna maendeleo ya mwanamke bila mwanaume.

Sauti ya Mratibu wa jinsia halmashauri ya jiji la Arusha Angelina Christian.

Naye Afisa maendeleo Habiba  Madebe amesema maswala ya kijinsia na maendeleo ya mwanamke hayawezi kusonga mbele bila kupata ushirikiano kutoka kwa wanaume.

Sauti ya Afisa maendeleo Habiba  Madebe