Savvy FM
Savvy FM
3 March 2026, 2:09 pm

Mkutano wa kimataifa wa mafunzo ya usawa na jinsia, ulemavu na ujumuishwaji wa kijamii umezikutanisha nchi zaidi ya 23 duniani lengo likiwa ni kujadili namna yakuendelea kuhudumia jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kwa makundi yenye mahitaji maalumu.
Na Mariam Mallya
Mara baada ya kufungua mkutano huo uliofanyika jijini Arusha, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu Dorothy Gwajima amesema dhumuni kubwa ni kujadili maswala ya usawa wa kijinsia kwa watu wenye ulemavu kwani mazingira yanapaswa kuwekwa vizuri kwa ajili yao ili waweze kufikia malengo yao.
Naye Mkurugenzi mkuu wa shirika la World vision Tanzania, James Anditi ameeleza umuhimu wa jukwaa hilo na kusema kuwa taifa haliwezi kusonga mbele kama halitowapatia watu wenye mahitaji maalum vipaumbele.
Jukwaa hilo la kimataifa linabebwa na kauli mbiu isemayo “Kubadili Mitazamo, Kuvunja Vikwazo na Kufungua Fursa,” hii ikitajwa kuchochea usawa wa kijinsia katika jamii kwa kuzingatia makundi yote muhimu kuanzia ngazi ya familia.