Savvy FM
Savvy FM
1 May 2026, 2:26 pm

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini Tanzania (RUJAT), Neville Meena, amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwani huwakutanisha wadau mbalimbali na wanahabari na kuwakubumbusha wanapaswa kufanya kazi kwa uhuru na bila kubugudhiwa.
Na Mariam Mallya
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika jijini Arusha, Neville Meena amesema uhuru wa vyombo vya habari unapaswa kuambatana na uwajibikaji wa kitaaluma kwa wanahabari kuzingatia misingi.
Aidha Bw.Meena waandishi wa habari wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo uchumi, kukamatwa na kusumbuliwa kwa kunyang’anywa vifaa vyao jambo ambalo linawafanya waandishi wa habari kushindwa kutekeleza majukumu yao
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa RUJAT, Prosper Kwigize, amesema kuwa uandishi wa habari ni ule unaogusa maslahi ya umma kwa kutatua changamoto za wananchi hasa kwa jamii za vijijini
Pia amesema kusema wananchi wa vijijini mara nyingi huathirika zaidi katika changamoto za amani na usalama, lakini bado wanakosa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika habari kutokana na changamoto za miundombinu ya mawasiliano na uwekezaji mdogo katika maeneo hayo.