

April 23, 2025, 1:56 pm
Kuelekea kilele cha siku ya maadhimisho ya kitaifa ya utoaji wa huduma za afya ya wanyama ambayo itafanyika April 26 mwaka huu,wadau na wafugaji wametakiwa kuacha tabia za kutumia dawa za ARV ili kunenepesha mifugo
Na Mzidalifa Saidi.
Akizungumza leo Daktari mkuu wa wanyama kutoka Halmashauri ya mji wa Babati Dkt Fatuma Mkombozi amesema kwa mkoa wa Manyara bado hawajapata kesi inayohusiana na matumizi ya ARV kwa mifugo na kusema wafugaji wa mijini wanapaswa kufuga michache ili iwe na tija.
Aidha,maadhimisho hayo ni ya tatu tangu kuanza na mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu inayosema “Mafanikio ya afya ya wanyama yanahitaji ushirikiano “
.