Savvy FM
Savvy FM
30 April 2026, 7:59 pm

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka 2026 yaendelea kuibua mijadala muhimu kuhusu mustakabali wa sekta ya habari nchini, huku wadau wakijadili kwa kina namna ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia ya kidigitali.
Na Mariam Mallya
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha, Mwenyekiti kutoka taasisi ya Tech and Media Convergence (TMC), Bi. Asha Abinallah Mkuruge amesema kuwa teknolojia ya akili bandia (AI) imechukua nafasi kubwa katika mijadala hiyo, ambapo imeelezwa kuwa inaweza kuwa fursa au changamoto kulingana na uelewa na matumizi yake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema sekta ya habari nchini inakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kupungua kwa mapato na mabadiliko makubwa ya teknolojia.
Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko amesema katika siku ya pili ya mijadala hiyo, wadau wameendelea kujadili hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini pamoja nakutoa wito kwa jamii kuheshimu taaluma ya uandishi wa habari na kufuata taratibu sahihi katika kushughulikia makosa ya wanahabari.