Savvy FM
Savvy FM
30 July 2026, 11:25 am

Wananchi wa kitongoji cha Olmesera kijiji cha Manyire kata ya Mlangarini mkoani Arusha ,wameamua kuchangishana shilingi elfu 70 kwa kila mwanakitongoji ili kuweza kununua eneo ambalo watajenga shule ya msingi na sekondari kwa ajili ya watoto wa kitongoji hicho.
Na Gasper Sambweti
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kitongoji wanakijiji hao wamesema wanaungana na mwenyekiti wa kitongoji ndugu Baraka ili kufikia malengo yao kwani watoto wao wanalazimika kutembea km20 kwa siku zikiwa km 10 kwenda ili kufika shule ya msingi na sekondari ya Mlangarini na km 10 kurudi ili kufika nyumbani.
Wananchi hao wamesema changamoto hiyo ya umbali wa shule ndio iliyopelekea kuamua kujichanga kama wanakijiji ili kujenga shule huku wakiiomba serikali kuwaunga mkono ili watoto wao waweze kupata elimu kwa urahisi kwani wanafunzi wengi wamekuwa wakikata tamaa yakuendelea na masomo huku wengine wakikumbana na vishawishi wakiwa njia wakielekea shuleni.